Swali: Swawm za wenye kuumikwa hii leo zinaharibika ikiwa wanatumia vifaa vya kisasa visivyonya damu?

Jibu: Hadiyth itabaki kama jinsi ilivyopokelewa. Kuharibika kwa swawm kwa sababu ametoa damu nje ni maelezo tu, kuna uwezekano ikawa si sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa salalm) amesema:

“Amevunja swawm mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa.”[1]

 Kwa hiyo na sisi pia tunasema kuwa swawm ya aliyefanya chuku na aliyefanyiwa imeharibika.

[1] Abu Daawuud (2367), at-Tirmidhiy (774), Ibn Maajah (1679) na Ahmad (15866). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (931).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (19) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtfq-22011435-01.mp3
  • Imechapishwa: 08/12/2019