Swawm ya Daawuud inapokutana na siku ya jumatatu, alkhami na masiku meupe

Swali: Kuna mtu anafunga siku moja na anakula siku nyingine. Siku ya kula kwake ikikutana na siku moja wapo ya masiku meupe au siku ya jumaatu au alkhamisi afunge siku hiyo au aendelee na swawm yake?

Jibu: Aendelee na swawm yake. Aendelee na nidhamu ya swawm yake ya kula siku moja na kufunga siku nyingine. Hili linatosheleza na masiku meupe. Kufunga siku moja na kula siku nyingine kunaingia ndani yake masiku ambayo imewekwa katika Shari´ah kuyafunga.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (54) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13468
  • Imechapishwa: 16/11/2014