Swawm ya ´Arafah inafuta madhambi makubwa?

Swali: Swawm ya siku ya ´Arafah ni kafara kwa madhambi makubwa?

Jibu: Hapana. Ni kafara ya madhambi madogo. Ama madhambi makubwa hayakafiriwi isipokuwa kwa Tawbah:

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ

“Mkijiepusha namadhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo.” (04:31)

“Swalah tano, Ijumaa mpaka Ijumaa na Ramadhaan mpaka Ramadhaan, ni kafara ya yaliyomo kati yake mtu akijiepusha na madhambi makubwa.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-14.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014


Takwimu
  • 27
  • 413
  • 1,821,446