Swali: Nasumbuliwa na kutokwa na manii katika siku za mchana wa Ramadhaan bila ya kuota wala kujichukua sehemu ya siri. Je, mambo haya yana taathira yoyote juu ya swawm?

Jibu: Ikiwa mambo ni kama ulivotaja basi kutokwa kwako na manii bila ya ladha mchana wa Ramadhaan hakuathiri swawm yako na wala huhitajii kulipa.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (10645)
  • Imechapishwa: 26/04/2020