Swawm ya ambaye ameshinda mchana mzima analala inasihi?

Swali: Je, swawm ya mtu mwenye kulala katika masiku ya Ramadhaan baada ya kula daku kisha akaswali swalah ya alfajiri na akalala mpaka wakati wa adhuhuri kisha akaswali na akalalala mpaka wakati wa alasiri  kisha akaswali na akalala mpaka wakati wa kufungua inasihi?

Jibu: Mambo yakiwa kama yalivyotajwa swawm ni sahihi. Lakini mfungaji kuendelea analala sehemu kubwa ya mchana ni kuzembea na khaswa khaswa katika mwezi wa Ramadhaan ambapo ni zama tukufu ambapo muislamu alitakiwa kufaidika katika mambo yatayomnufaisha katika kusoma Qur-aan kwa wingi, kutafuta riziki na kujifunza elimu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/302)
  • Imechapishwa: 09/06/2017