Swawm na swalah za pamoja ni Bid´ah


Swali: Ni ipi hukumu ya swawm ya pamoja?

Jibu: Ni Bid´ah. Swawm ya pamoja ni Bid´ah. Swalah za pamoja usiku kwa kuambizana hilo watu waamke usiku ili waswali swalah ya pamoja… Swalah ya pamoja na sio swalah ya Jamaa´ah, yaani swalah ya pamoja, bi maana wewe unaswali kwenye chumba chako, mwingine kwenye chumba chake namna hii. Au wanasimama sehemu moja na kila mmoja anaswali peke yake, hili halijuzu. Hii ni katika Bid´ah iliyozushwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (69) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13888
  • Imechapishwa: 16/11/2014