Muislamu anatakiwa kufunga kwa kumtakasia Allaah nia hali ya kuwa ni mwenye kutaka uso wa Allaah na nyumba ya Aakhirah. Mtu akifunga kwa ajili ya Allaah basi anastahamili ule uzito wa kuacha chakula na kinywaji. Muisalmu anayastahamili. Bali hakika ya muislamu anahisi ladha kwa mambo haya. Utamuona kuwa ni mwenye kuhisi ladha kwayo kwa sababu anajua kuwa ni kumtii Allaah, anamridhisha Mola wake (´Azza wa Jall), anatekeleza wajibu na anajua kuwa thawabu za Allaah ndio bora na tukufu zaidi. Muumini utamuona kuwa anahisi ladha kwa ´ibaadah japokuwa mwili unateseka. Ni kweli kwamba mwili unachoka na kuteseka. Lakini hata hivo moyo uko ndani ya neema. Ugumu na uzito huu si lolote si chochote kwa muumini.Utamuona muumini kuwa ni mwenye njaa lakini hata hivo ni mwenye furaha, kustareheka, moyo wake uko ndani ya neema na furaha. Muumini anajua kuwa yaliyoko kwa Allaah ndio matukufu zaidi na yenye kubaki, anajua kuwa Allaah atamnywesha kutoka kwenye hodhi/birika la Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba ipo siku ataambiwa:

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ

”Kuleni na kunyweni hali ya kuwa ni wenye furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilopita.”[1]

[1] 69:24

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://shrajhi.com.sa/uploads/rmadhan_02.mp3
  • Imechapishwa: 06/05/2019