Swali: Mimi nina mke ambaye ana miaka takriban themanini na tano. Ni mwanamke wa Kiislamu na wa kheri. Mwishoni mwa umri wake alipatwa na maradhi ya kisukari na udhaifu kufikia mpaka kwamba baadhi ya siku akalazwa hospitali kwenye koma na siku zengine akalazwa nyumbani. Hawezi kuzungumza vizuri na wakati mwingine hakijui kile anachokitamka na wala hawezi kutembea isipokuwa mpaka awe na wenye kumsaidia, kumnyanyua katika watoto wake. Tatizo ni kwamba hakuswali kwa muda wa miaka miwili. Inapokuja katika swawm sisi tunamlishizia. Jengine ni kwamba hajui nyakati za swalah na hajui ni kipi anachotakiwa kusema katika swalah na pia kujigonga katika maneno yake ni kwingi kuliko usawa. Tunaomba utujibu juu ya tatizo hili. Je, ni wajibu kwake kuswali pamoja na kuwa na kasoro kwenye akili? Ni wajibu kwetu kumlishizia Ramadhaan badala ya kufunga? Ni yepi yanayotuwajibikia sisi katika yale yanayomlazimu?

Jibu: Mambo yakiwa hivo mlivyoeleza basi hailazimu kufunga wala kuswali.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/168-168)
  • Imechapishwa: 04/06/2017