Swawm inakatwa pale jua linapozama

Swali: Katika mji wetu wanaadhini dakika tano baada ya kuzama kwa jua. Inajuzu kwetu kukata swawm kabla ya adhaana?

Jibu: Kukata swawm kunakuwa kwa kuzama kwa jua. Ikiwa mnaona kuwa jua limeshakwishazama basi kateni swawm sawa ikiwa wameshaadhini au bado. Ama ikiwa hamuoni jua basi msifuturu mpaka muadhini aadhini. Hili ni salama zaidi kwenu ili msije kukata swawm kabla ya jua kuzama.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (22) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsirayat-05-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 19/06/2020