Swali: Swawm ina nafasi gani katika Uislamu?

Jibu: Nafasi ya swawm katika Uislamu ni kwamba ni moja katika nguzo zake kubwa. Uislamu hausimama na wala hautimii isipokuwa kwa swawm.

Kuhusu fadhila yake katika Uislamu, imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ?alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayefunga Ramadhaan kwa imani na kwa matarajio basi atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”[1]

[1] al-Bukhaariy (1901) na (2014) na Muslim (760).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/12)
  • Imechapishwa: 29/05/2017