Swawm imeharibika baada ya kutaniatania na mke kutokwa na madhiy?


Swali: Siku moja wapo ya Ramadhaan nilikuwa nimekaa pembezoni na mke wangu ilihali sote tumefunga. Nilikaa naye karibu nusu saa ambapo tulikuwa tukifanyiana mzaha. Baada ya kutoka pale nikakuta kwenye suruwali yangu tone la majimaji limetoka kwenye dhakari yangu. Jambo hilo lilijikariri kwa mara ya pili. Naomba unifaidishe: je, nawajibika kutoka kafara?

Jibu: Mambo yakiwa kama ulivyosema hakuna kwako kulipa wala kutoa kafara kwa kuzingatia kubaki juu ya msingi. Isipokuwa tu ikithibiti kuwa tone la majimaji hayo ilikuwa ni manii. Katika hali hiyo itakuwajibu kuoga na kulipa pasi na kutoa kafara.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/273)
  • Imechapishwa: 11/06/2017