Swawm iliyopendekezwa tarehe 29 na 30 Sha´baan

Swali: Mke wangu anafunga alkhamisi na siku ya jumatatu. Anauliza kama inafaa kwake kufunga kabla ya kuingia mwezi [wa Ramadhaan]?

Jibu: Afunge. Hiyo ni ada yake. Ambaye amezowea kufunga swawm fulani afunge. Lakini ambaye alikuwa hana ada ya kufunga asifunge. Nakusudia asifunge tarehe 30 wala tarehe 29 Sha´baan. Asifunge baada ya nusu Sha´baan. Lakini ambaye alikuwa na mazowea ya kufunga hapana vibaya. Ni kama ambaye amezowea kufunga siku moja kula siku ya kufuatia, anafunga jumatatu na alkhamisi. Mtu huyu ana ruhusa ya kuendelea kufunga. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili, isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm. Basi aiendeleze.”[1]

[1] al-Bukhaariy (1914) na Muslim (1082).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21692/حكم-صيام-اخر-شعبان-لمن-له-عادة-صوم
  • Imechapishwa: 19/09/2022