Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ

“Simamisheni swalah na toeni zakaah na rukuuni pamoja na wanaorukuu.”[1]

Simamisheni swalah kwa dhahiri na kwa kujificha na mtoe zakaah kuwapa wale wenye kuiistahiki. Maneno Yake:

وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ

“… na rukuuni pamoja na wanaorukuu.”

Bi maana swalini pamoja na waswaliji. Mkifanya hivo pamoja na kuwaamini Mitume na Aayah za Allaah, basi mtakuwa mmekusanya kati ya matendo ambayo ni ya dhahiri na yaliyojificha, kumtakasia nia Muumba na kuwatendea wema waja Wake, ´ibaadah za kimoyo, za kimwili na za kimali. Maneno Yake:

وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ

“… na rukuuni pamoja na wanaorukuu.”

Bi maana swalini pamoja na waswaliji. Hapa kuna amri ya wanamme kuswali kwenye mkusanyiko na kwamba jambo hilo ni lazima. Faida nyingine tunapata ni kwamba Rukuu´ ni nguzo miongoni mwa nguzo za swalah kwa sababu ameielezea swalah kwa Rukuu´.  Kuelezewa ´ibaadah kwa sehemu yake ni jambo linalojulisha juu ya ufaradhi wake.

[1] 02:43

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 42
  • Imechapishwa: 01/07/2020