Swali Tarawiyh nyuma ya imamu hadi mwisho

Swali: Baadhi ya watu wanaswali Tarawiyh nyuma ya imamu. Lakini imamu anaposimama kuswali Witr wanajitenga na imamu.

Jibu: Huku ni kwenda kinyume na Sunnah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule atakayesimama pamoja na imamu mpaka akamaliza, basi anaandikiwa usiku mzima.”

Yule anayetaka kupata thawabu kamilifu kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) asijitenge na imamu.

Kama anataka kuendelea kusimama mwishoni mwa usiku afanye hivo hata kama ni baada ya kuswali Witr pamoja na imamu. Asimame tena nyumbani kwake na wala asikariri Witr kwa mara nyingine. Ile Witr aliyoswali pamoja na imamu inamtosha. Baadhi ya watu wanajitenga na imamu kwa hoja eti wataswali mwishoni mwa usiku na kwamba wanachelewesha Witr mpaka mwishoni mwa usiku. Huku ni kwenda kinyume na kilicho bora zaidi. Bora ni yeye kusimama pamoja na imamu mpaka amalize kuswali Witr pamoja na imamu. Akisimama mwishoni mwa usiku hahitajii kuswali Witr nyingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=2vQdgZLzLuI
  • Imechapishwa: 11/05/2020