Swali kama hili halitakiwi kuwepo Saudi Arabia


Swali: Niliswali msikiti mmoja. Kijana mmoja akaniona, akanisalimia na kuniuliza mimi ni katika kundi gani. Nikamwambia kwamba sote ni ndugu waislamu. Hakukubali jibu. Akashikilia na kusema ni lazima niwe katika Ahl-ul-Hadiyth, Jamaa´at-ut-Tabliygh au al-Ikhwaan al-Muslimuun. Baadaye ikaja kubainika kwamba kijana huyo sio katika watu wa msikiti huo na wala haswali hapo. Wakati wa kuswali ulipofika akasema kuwa yeye haswali nyuma ya mtu mpaka pale atakapojua ni katika kundi gani. Wewe na ndugu wengine wanajua namna ambavo mipasuko hii imesababisha shari kubwa na tofauti kati ya ndugu na wanafunzi. Tunatarajia nasaha zako.

Jibu: Naonelea kuwa mfano wa sulubu kama hizi zinatakiwa kuteketezwa. Watu wote wako sawa na himdi zote njema ni za Allaah. Watu wote ni waislamu. Jawabu lako ni sahihi kabisa.

Ama kuwalazimisha watu wagawanyike mapote mpaka iwe Tabliyghiyyuun, Suufiyyah, al-Ikhwaan al-Muslimuun, Ishaahiyyuun, Ahl-us-Sunnah na kadhalika, ni kitu ambacho nchi yetu haikihitajii. Pengine nchi zengine zinahitajia jambo hilo. Kwa sababu huko kuna makundi mengi. Lakini huku kwetu himdi zote ni za Allaah kwamba hakipo.

Hawa ambao wanaita katika Hizbiyyah, uvyamavyama, wanajidhuru wao wenyewe na ndugu zao wengine. Wataipelekea nchi katika mgogoro mrefu na kuwepo kwa mapote mengi.

Nasaha zangu kwa ndugu ni yeye amwombe Allaah msamaha na atubie Kwake. Anatakiwa kutambua kwamba sote ni ndugu juu ya dini moja, chini ya kivuli cha Shari´ah moja. Ama kumlazimisha mtu na kusema kwamba ni lazima uwe katika al-Ikhwaan, Tabliyghiyyuun au Ahl-ul-Hadiyth? Sote tunazifata Hadiyth na Qur-aan. Tunamuomba Allaah aongoze wote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (60 B)
  • Imechapishwa: 16/07/2021