Swalah ya sunnah ndani ya gari mjini


Swali: Je, inajuzu kuswali swalah ya Sunnah ndani ya gari katika mji mtu anapoishi?

Jibu: Swalah ya Sunnah ndani ya gari inaswaliwa katika safari, kama ambavyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akifanya. Isiswaliwe kwenye vipando ndani ya mji sawa iwe ni gari au mnyama. Hakuna dalili ya hili. Isipokuwa safarini tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 28/05/2018