Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali Rakaa ngapi baada ya Swalah ya Ijumaa? Tunaomba faida.

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah ni kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali baada ya Ijumaa Rakaa mbili nyumbani kwake. Namna hii ndivyo ilivyokuja katika Swahiyh al-Bukhaariy na Muslim, Hadiyth ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

“Alikuwa akiswali Rakaa mbili baada ya Ijumaa nyumbani kwake.”

Lakini, kasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kuswali baada ya Ijumaa, aswali (Rakaa) nne.”

Wanasema wanachuoni, kuoanisha baina ya Hadiyth hizi mbili ni kuwa, akiswali Msikitini ataswali Rakaa nne, na akiswali nyumbani kwake ataswali Rakaa mbili. Kuoanisha baina ya nususi hizi mbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb (770)
  • Imechapishwa: 12/03/2018