Swalah ya mwenye kuswali kikamilifu nyuma ya msafiri

Swali: Umetaja katika moja ya mihadhara yako iliyotangulia kwamba mtu akisafiri umbali wa takriban 20 km basi inafaa kwake kufupisha swalah kwa sharti asikae huko chini ya siku mbili. Mtu akiwa haoni kwamba inafaa kufanya hivo na akasafiri na watu wenye kuona kufaa kufupisha swalah inafaa kwake kuswali kikamilifu au anazingatiwa kwamba anaenda kinyume na mkusanyiko?

Jibu: Hakuna neno akaswali kikamilifu. Midhali masuala haya kuna tofauti ndani yake na yeye haoni kwamba inafaa kwake kufupisha, basi aswali nyuma ya imamu ambaye anafupisha swalah. Atapomaliza kuswali nyuma ya imamu wake basi asimame na kuswali Rak´ah zengine mbili. Katika hali hii ikiwa huyu ambaye anaona kuwa haifai kufupisha swalah ndiye msomi zaidi katika wao, basi yeye ndiye awe imamu wao. Ikiwa yeye ndiye atakuwa imamu wao basi italazimika kwa wote kukamilisha swalah. Kwa sababu msafiri akiswali nyuma ya imamu anayeswali kikamilifu basi na yeye pia atalazimika kuswali kikamilifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1453
  • Imechapishwa: 04/01/2020