Swalah ya mwanamke pindi mwanamme anapita mbele yake

Swali: Je, swalah ya mwanamke inaharibika kwa mwanamme au mwanamke kupita mbele yake ni mamoja ni katika jamaa zake au watu wengine?

Jibu: Mwanamme kupita mbele hakuharibu swalah ya mwanamke. Lakini haijuzu kwake kupita mbele ya mwenye kuswali au kati yake yeye na Sutrah yake. Ni mamoja mswaliji ni mwanamme au mwanamke. Kinachoharibu swalah ni mwanamke, punda na mbwa mweusi. Hivo ndivo zilivyosihi Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Abu Dharr, Abu Hurayrah na Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhum).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/90)
  • Imechapishwa: 10/10/2021