Swalah ya mwanamke ndani ya nyumba iliyoambatana na msikiti

Swali: Ikiwa nyumba iko karibu na msikiti na vimekamatana na hakuna kati yake na wanakoswali wanawake isipokuwa wanamme peke yake. Aidha nyuma iko iko ndani ya ukuta wa msikiti. Je, inafaa kwa mwanamke katika hali hii kuswali pamoja na imamu?

Jibu: Kilichoko ndani ya msikiti hakiitwi nyumba. Bali ni sehemu ya msikiti. Kila kilichokuwa ndani ya ukuta wa msikiti ni sehemu katika msikiti. Wanawake wakifanyiwa nyuma ya msikiti mahali pa kuswalia ni sehemu katika msikiti.

Lakini maeneo hayo yakiwa nje ya msikiti basi hapana hukumu moja ya msikiti. Kwa ajili hiyo ikiwa nyumba iko nje ya msikiti basi inafaa kwa mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi kukaa mahali hapo na kusikiliza Khutbah au darsa. Lakini haifai kwake kufanya hivo ikiwa nyumba hiyo iko ndani ya ukuta wa msikiti.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 11/09/2021