Swalah ya mwanamke hali ya kufunika uso na vifuniko vya mikono

Swali 259: Je, inajuzu kwa mwanamke kuswali akiwa na Niqaab na vifuniko vya mikono?

Jibu: Ikiwa mwanamke anaswali nyumbani kwake au sehemu ambayo hawaingii isipokuwa tu wale wanaume ambao ni Mahram zake, basi kilichowekwa katika Shari´ah ni yeye kuacha wazi uso wazi na mikono. Lengo ni ili paji la uso na pua viweze kugusa sehemu ile ya kusujudia. Vivyo hivyo vitanga vya mikono.

Ama akiwa anaswali na pembezoni mwake kuna wanaume wasiokuwa Mahram zake basi ni lazima kufunika uso wake. Kwa sababu kufunika uso wake mbele ya wasiokuwa Mahram zake ni lazima. Haifai kwake kuufunua mbele zao, kama ilivyofahamisha hivo Qur-aan, Sunnah na mtazamo sahihi usiyopingana na akili seuze muumini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 99
  • Imechapishwa: 01/10/2019