Swalah ya mwanamke haisihi mpaka awe na hina?

Swali: Nimewasikia baadhi ya watu wakisema kwamba haijuzu kuswali isipokuwa [mwanamke] akiwa na hina. Je, ni kweli? Vilevile wanasema kuwa mwenye kufa na mikononi mwake hakuna hina basi haswaliwi kwa sababu mikono yake imefanan na ya wanaume.

Jibu: Haya si kweli. Hina sio katika mambo yaliyofaradhishwa wala katika mambo ya lazima mpaka ifikie katika ngazi hii. Mwanamke asipopaka hina hakusemwi kuwa amekosea au ametenda dhambi. Kadhalika hakusemwi kwamba akifa haswaliwi au kwamba swalah yake haikubaliwi. Haya ni miongoni mwa mambo yanayosikiwa na watu wasiokuwa na elimu kutoka midomoni mwao au kutoka tu kwa watu wanaodhani kuwa ni wanachuoni ilihali sio wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (13) http://binothaimeen.net/content/6774
  • Imechapishwa: 25/01/2021