Swali: Je, ni kweli kwamba swalah ya aliyeswali na vazi lenye kuvuka kongo mbili za miguu ni batili?

Jibu: Hapana, sio batili. Kumepokelewa Hadiyth ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona mtu ambaye ni musbil ambapo akamuamrisha airudi swalah yake. Lakini hata hivyo huenda (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia hivo kwa sababu ya kasoro zilizokuwemo katika swalah ya mtu huyo mbali na Isbaal.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (82) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-08-3-1439-01.mp3