Swalah ya msafiri nyuma ya imamu mkazi


Swali: Inajuzu kwa msafiri kufupisha swalah akiswali nyuma ya imamu ambaye ni mkazi?

Jibu: Hapana. Hukumu yake ni kama hukumu ya imamu. Imamu hakuwekwa isipokuwa ili tu afuatwe. Kwa hivyo ni lazima akamilishe swalah yake na imamu ambaye ni mkazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (66) http://alfawzan.af.org.sa/node/16524
  • Imechapishwa: 13/08/2017