Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mkusanyiko kwa mwanamke shuleni?

Jibu: Swalah ya mkusanyiko kwa mwanamke sio lazima. Lakini hapana vibaya wakiswali pamoja ili baadhi wajifunze kutoka kwa wengine na wafaidishane. Imepokelewa kutoka kwa Umm Salamah na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba waliwaswalisha baadhi ya wanawake. Ni jambo linalojulikana kuwa kitu hicho kina fadhilah na manufaa ikiwa kati yao kuna mwanamke mwenye elimu anayewaswalisha na wanafaidika sana kutoka kwake na wanajifunza kutoka kwake namna ya kuswali. Mwanamke huyo anayewaswalisha atasimama katikati yao na si mbele yao na atasoma kwa sauti ya juu katika zile swalah za kusoma kwa sauti ya juu. Hicho ni kitu kinachopendeza ikiwepesika kufanya hivo na si lazima. Swalah ya mkusanyiko inawalazimu wanamme katika nyumba za Allaah (Ta´ala) kwa ajili ya kutendea kazi dalili za ki-Shari´ah. Kuhusu wanawake swalah zao nyumbani ni bora kwao. Ni mamoja wanaswali mmojammoja au kwa pamoja.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/77)
  • Imechapishwa: 18/08/2022