Swali: Ni vipi viziwi na mabubu watamfata imamu wao? Ni wenye kusamehewa wakijitahidi katika kufata?

Jibu: Kiziwi na bubu wanaona kule kuhama kutoka hapa na pale. Wakiwa pamoja na waswaliji wengine basi wawafate. Na wakiwa wanamuona imamu basi wamfuate. Hii ni moja ya faida ya kunyanyua mikono. Wamesema baadhi yao kwamba miongoni mwa faida za kunyanyua mikono wakati wa Takbiyr ni ili kiziwi apate kuona. Kuhusu kipofu yeye anasikia kunaposemwa “Allaahu Akbar”. Kiziwi anapomuona imamu ananyanyua mikono ilihali yuko mbali, basi atatambua kuwa imamu amesema “Allaahu Akbar”. Wakikusanyika viziwi na mabubu na imamu akawa ni mmoja wao, hali hiyo ni nadra sana kutokea. Lakini kiziwi na bubu wakiwa pamoja na waswaliji wengine basi amfate imamu na waswaliji wengine. Swali liko wazi kwamba wote walikuwa ni viziwi na mabubu na imamu alikuwa ni mmoja katika wao. Watayajua hayo kwa zile ishara.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 12/06/2021