Swali: Kuna bwana mmoja ni kiziwi na bubu anayeswali na hajui sharti za swalah. Je, inasihi swalah yake?

Jibu: Aswali kulingana na hali yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Ikiwezekana basi afunzwe kwa ishara au kwa njia yoyote anayoijua. Isipowezekana hakuna kinachomlazimu isipokuwa kile alichojua. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا

”Hatukuwa Wenye kuadhibu mpaka tumtume Mtume.”[2]

Kama anaweza kufunzwa kwa kuandika kwa sababu ni mwenye kuona anaweza kusoma maandishi, basi ni lazima kumfunza kwa kuandika. Kwa sababu kumfunza mjinga ni jambo la lazima kwa waislamu na kwa wanafunzi. Afunzwe kwa njia inayowezekana; kwa ishara na uandishi mpaka itakasike dhimma yake na aitambue dini yake.

[1] 64:16

[2] 17:15

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/370)
  • Imechapishwa: 26/09/2021