Swalah ya ´iyd wakati wa janga la corona

Swali: Ni vipi itaswaliwa swalah ya ´iyd kwa mnasaba huu wa janga la corona?

Jibu: Ikishindikana kuswali swalah ya ´iyd kwa sababu ya kikwazo, kama ilivyo hii leo, basi hukumu yake ni kama ya yule ambaye amepitwa na swalah ya ´iyd. Wanachuoni wana maoni mbalimbali juu ya suala hili:

1- Itaswaliwa Rak´ah mbili.

2- Itaswaliwa Rak´ah nne.

3- Itaswaliwa kawaida. Maoni haya ndio sahihi.

Kwa maana nyingine ni kwamba itaswaliwa Rak´ah mbili, Takbiyr za ziada na atasoma kwa sauti ya juu. Asitowe Khutbah. Ni kama mfano wa ´ibaadah zengine zote zinapokidhiwa hii pia itakidhiwa kawaida kama ilivyo. Aidha inaweza kuswaliwa na mmojammoja na kundi mkusanyiko. Dalili juu ya hilo ni kwamba Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) alipitwa na swalah ya ´iyd, ambapo akawakusanya wakeze na wanawe kisha akamfanya mtumwa wake aliyemwacha huru ´Abdullaah bin Abiy ´Utbah akawaswalisha Rak´ah mbili na akaleta Takbiyr za ziada, kama ilivyo swalah ya kawaida mijini.

Kuhusu maoni yanayosema kuwa swalah ya ´iyd haikidhiwi, si muhimu kuileta hapa. Kwa sababu katika hali yetu hivi sasa swalah ya ´iyd haitoswaliwa kabisa na hivyo ina maana kwamba kutaachwa kuswaliwa faradhi. Lakini hata hivyo katika hali hii swalah ya ´iyd italinganishwa na swalah ya ´iyd iliyompita mtu – na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir al-Barraak
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://sh-albarrak.com/article/18234
  • Imechapishwa: 23/05/2020