Swalah ya ijumaa kwenye ukumbi wa semina


Swali: Nilikuwa kwenye semina katika moja ya nchi za kiarabu kwa siku tano. Tukaswali swalah zote kwenye ukumbi wa semina kwa sababu pambizoni mwetu hapakuwepo misikiti. Wakaniteua mimi kuwa imamu ambapo nikawatolea Khutbah na kuwaswalisha swalah ya ijumaa kwenye ukumbi huohuo. Kitendo changu kilikuwa cha sawa?

Jibu: Hawa sio wakazi. Swalah ya ijumaa haikufanywa katika mji. Ikiwa kuna sehemu ya karibu panaposwaliwa ijumaa, waswali pamoja na waislamu. Ikiwa hapaswaliwi swalah ya ijumaa na ilihali ni wasafiri, hawaswali swalah ya ijumaa. Ikiwa kuna karibu nao kuna msikiti, waswali swalah ya ijumaa ndani yake. Ikiwa hakuna msikiti wowote, waswali Dhuhr na wasiswali swalah ya ijumaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/de
  • Imechapishwa: 01/10/2017