Swalah ya idi inawalazimu wanamme na wanawake

Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya ´iyd? Ni vipi kumjibu anayewazuia wanawake na wasichana zake kushuhudia kwa hoja ya wao kuepuka kusongamana na wanamme?

Jibu: Hukumu yake ni lazima kwa wanamme na wanawake. Ni juu ya wanawake wenye hedhi kuhudhuria na washuhudie mkusanyiko [wa waislamu]. Kuhusu msongamano unaweza kuepukwa kwa mfano kwa kutembea kwa miguu au wakachukua njia nyingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 176
  • Imechapishwa: 03/07/2022