Swalah ya Ibraahiymiyyah inatakiwa kusomwa pia katika Tashahhud ya kwanza

Swali: Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) ametaja kwamba miongoni mwa mambo yanayopendeza ya swalah ni kusoma swalah ya Ibraahiymiyyah katika Tashahhud ya kwanza baada ya Rak´ah mbili katika Dhuhr, ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa. Je, kuna dalili juu ya hilo?

Jibu: Maswahabah walipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakasema:

“Tumejua namna ya kukuswalia. Ni vipi tutakutakia amani?”

Akawaelekeza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah ya Ibraahiymiyyah. Hapa hakuna kinachofahamisha ni katika Tashahhud ya mwisho peke yake. Hapa kuna dalili kwamba haya yanafanywa katika Tashahhud. Kunaingia Tashahhud ya kwanza na ya mwisho. Isipokuwa tu wanazuoni wamesema kuwa Tashahhud ya kwanza imejengeka juu ya kuwepesisha na hivyo haitosomwa. Vinginevyo hakuna yanayofahamisha kubagua Tashahhud ya kwanza. Msingi ni kwamba swali walilouliza kunaingia Tashahhud ya kwanza na ya mwisho. Huo ndio msingi wa dalili. Anayebagua Tashahhud ya kwanza ndiye ambaye anatakiwa kuombwa dalili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Kariym bin ´Abdillaah al-Khudhwayr
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://saif.af.org.sa/sites/default/files/05_28.mp3
  • Imechapishwa: 12/09/2022