Swalah ya faradhi nyuma ya anayeswali swalah ya sunnah


Swali 223: Ni ipi hukumu ya swalah ya faradhi nyuma ya anayeswali swalah ya sunnah kama ambaye anaswali swalah ya faradhi nyuma ya anayeswali swalah ya Tarawiyh?

Jibu: Hakuna neno kuswali ´ishaa nyuma ya anayeswali Tarawiyh. Imaam Ahamad (Rahimahu Allaah) amelitaja hilo. Akiwa ni msafiri na akajiunga pamoja na imamu kuanzia mwanzoni mwa swalah, basi atatoa salamu pamoja naye. Vinginevyo atakamilisha Rak´ah zenye kubak pale imamu atapotoa salamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 306
  • Imechapishwa: 18/05/2019