Swalah ya anayeswali Dhuhr nyuma ya anayeswali ´Aswr ni sahihi?

Swali: Mtu akiswali Dhuhr nyuma ya imamu anayeswali ´Aswr swalah yake ni sahihi?

Jibu: Mtu akiswali Dhuhr nyuma ya imamu anayeswali ´Aswr hakuna neno na swalah yake ni sahihi kwa mujibu wa maoni yenye nguvu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kila kitendo kinategemea nia na kila mmoja atalipwa kwa lile alilonuia.”

Hakukuthibiti kitu kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kinachofahamisha ya kwamba nia ya imamu na mswaliji zinapaswa kuafikiana. Kwa hivyo kila mmoja anakuwa na nia yake kama inavyofahamisha Hadiyth:

“… na kila mmoja atalipwa kwa lile alilonuia.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/446)
  • Imechapishwa: 23/07/2017