Swalah ya anayeburuta nguo ni sahihi?


Swali: Kuburuza nguo kunabatilisha swalah?

Jibu: Mwenye kuruza nguo hakuna shaka kwamba amefanya dhambi kubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kilichoko chini ya fundo mbili za miguu ni Motoni.”

Wanachuoni wametofautiana juu ya kusihi kwa swalah yake. Kuna wanaosema kuwa swalah yake ni sahihi pamoja na kuwa anapata dhambi kwa kuburuza nguo yake. Wengine wakasema kuwa swalah yake sio sahihi kwa kuwa amevaa nguo ya haramu.

Maoni yenye nguvu ni kwamba swalah yake ni sahihi. Lakini hata hivyo anapata dhambi kwa kuvaa nguo inayovuka kongo mbili za miguu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (16)
  • Imechapishwa: 19/11/2017