Swalah ya ambaye anahisi kutokwa na mkojo wakati fulani


Swali: Nahisi kutokwa na mkojo baada ya kuosha na maji. Wakati fulani nahisi kutokwa na mkojo na nikitazama naona mkojo kweli na wakati mwingine nahisi kutokwa na mkojo na nikitazama sipati na hivyo naenda kuswali. Ni ipi hukumu ya swalah yangu?

Jibu: Ikiwa mtu anajua kuwa anatokwa na matone bora ni yeye kutofanya haraka. Bora ni yeye kuchelewa kidogo mpaka ayakinishe kweli kuwa matone yametoka. Ama ikiwa inahusiana na mambo ya mashaka anatakiwa kuachana nayo. Iwapo atanyunyizia maji juu ya tupu ili kukata wasiwasi itakuwa ni bora zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2018