Swalah ya aliyesilimu bila ya al-Faatihah

Swali: Kuna mtu aliingia katika Uislamu na ukafika wakati wa swalah. Alikuwa hajahifadhi kitu katika Qur-aan na anahitaji muda kidogo. Je, inajuzu kwake kuswali kama alivyo au ni lazima kwake kuhifadhi Qur-aan?

Jibu: Aswali na wale waislamu walioko pale. Aswali hata kama hakuhifadhi kitu katika Qur-aan. Asiache swalah. Ikiwa hakuna mtu mwenye kuswali, aswali vivyo hivyo kadri na anavyoweza. Ikiwa anajua kitu katika Qur-aan, akisome. Vinginevyo amhimidi Allaah, aseme kuwa Allaah ni mkubwa na aseme kuwa hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Kisha arukuu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (6) http://alfawzan.af.org.sa/node/14379
  • Imechapishwa: 08/12/2016