Swali: Wengi wanaswali Ramadhaan peke yake. Ni kipi unachowanasihi?

Jibu: Nawanasihi kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika wakati wote, katika Ramadhaan na kwenginepo. Mtu ameamrishwa kumcha Allaah mpaka wakati wa kuaga dunia. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ

“… na mwabudu Mola wako mpaka ikufikie yakini.” (15:99)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/117)
  • Imechapishwa: 30/04/2021