Swali: Je, inafaa kuswali nyuma ya mshirikina?

Jibu: Ambaye ni kafiri kwa njia ya kwamba anamwabudu asiyekuwa Allaah na anataka uokozi viumbe katika yale mambo asiyoyaweza yeyote asiyekuwa Allaah, huyo hausihi uimamu wake. Hatakiwi kuwaongoza waislamu isipokuwa muislamu tu. Ambaye anamwabudu mwingine asiyekuwa Allaah, anamuwekea nadhiri mwingine asiyekuwa Allaah na anachinja kwa ajili ya mwingine asiyekuwa Allaah ni kafiri na mshirikina. Haijuzu akawaswalisha waislamu kwa sababu sio muislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/حكم-الصلاة-خلف-المشرك
  • Imechapishwa: 20/06/2022