Swali: Niliswali nyuma ya Imamu na mimi nilikuwa katika safari. Imamu huyu hakunyanyua mikono yake wakati alipofungua Swalah kwa Takbiyr ya kwanza. Je, Swalah yangu ni sahihi?

Jibu: Kunyanyua mikono ni Sunnah na sio lazima. Baadhi ya wanachuoni wanaonelea hakuna kunyanyua mikono. Lakini Sunnah ni kunyanyua mikono wakati wa kufunga Swalah, kwenda katika Rukuu na wakati wa kuinuka kutoka kwenye Rukuu. Hii ndio Sunnah. Lau hakunyanyua hana juu yake kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (64) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13821
  • Imechapishwa: 16/11/2014