Swalah nyingi za ´iyd katika msikiti mmoja


Swali: Sisi tunaishi katika moja ya nchi za kikafiri. Tuko wengi lakini misikiti ni michache. Tunapata ugumu katika kutekeleza swalah za ´iyd mbili. Hatuwezi kufanya swalah ya mkusanyiko mmoja kutokana na wingi wa watu. Vilevile hatuwezi kuswali nje ya msikiti. Je, tunaweza kutekeleza swalah ya ´iyd katika msikiti mmoja mara mbili au mara tatu kwa Khutbah yenye maudhui tofauti?

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninapokuamrisheni jambo basi lifanyeni muwezavyo.”[2]

Mkiweza kutekeleza swalah ya ´iyd kwa pamoja katika jangwani ndio Sunnah. Msipoweza basi inatosha wakipatikana miongoni mwenu watakaoweza kuhudhuria swalah hiyo.

[1] 64:16

[2] al-Bukhaariy (7288).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 42
  • Imechapishwa: 16/06/2021