Swalah nyingi za faradhi kwa wudhuu´ mmoja II

Swali: Nikitawadha na nikakusudia kwa wudhuu´ wangu kuswali ´Aswr na nikaswali na nikabaki na twahara mpaka magharibi. Je, inafaa kuswali Maghrib kwa twahara ya swalah ya ´Aswr?

Jibu: Hakuna kikwazo cha kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali siku ya Ufunguzi wa Makkah swalah tano kwa wudhuu´ wa swalah ya Fajr kukiwemo Dhuhr na ´Aswr. Wakati ´Umar alipomuuliza akasema:

“Nimefanya kwa makusudi, ee ´Umar.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/هل-يجوز-الوضوء-الواحد-لكثر-من-صلاة
  • Imechapishwa: 19/06/2022