Swalah nne kwa wudhuu´ mmoja


Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuswali faradhi nne kwa wudhuu´ mmoja?

Jibu: Hakuna neno. Hakuna neno kwa wudhuu´ mmoja mtu akaswali swalah nne au zaidi.

Mwendasha kipindi: Lakini bora ni yeye kutawadha au aendelee na wudhuu´ huohuo?

Jibu: Akitawadha tena ndio vyema na bora zaidi. Kwa sababu ni kufanya upya wudhuu´ akatawadha kwa ajili ya kila swalah. Asipotawadha hakuna neno kwake, kwani hayo yamethibiti kutoka katika matendo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (15) http://binothaimeen.net/content/6792
  • Imechapishwa: 13/02/2021