Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa suruwali khaswa baadhi ya wanaoivaa inaonekana sehemu ya ´awrah zao wanapokuwa wamerukuu na wamesujudu ndani ya swalah?

Jibu: Ikiwa suruwali inafunika kati ya kitovu na magoti kwa mwanamme, pana na si yenye kubana basi itasihi kuswali ndani yake. Ingawa bora juu yake kuwe kanzu inayofunika yaliyo kati ya kitovu na magoti na inashuka kutoka hapo mpaka kwenye nusu ya muundi au kwenye vifundo vya miguu. Kufanya hivo ndio kamilifu zaidi katika kufunika.

Kuswali ndani ya kikoi kinachofunika vizuri ndio bora zaidi kuliko kuswali kwenye suruwali ikiwa juu yake hakuna kanzu inayofunika. Kikoi ni kamilifu zaidi katika kusitiri kuliko suruwali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/414)
  • Imechapishwa: 03/10/2021