Swalah na kusengenya watu


Swali: Ni ipi hukumu kwa wale wanaoswali na mkusanyiko misikitini lakini hata hivyo wanajishughulisha na maneno ya kipuuzi na kusengenya na kueneza uvumi kati ya watu?

Jibu: Kule kuswali kwao na mkusanyiko msikitini wametekeleza faradhi. Wameitekeleza na himdi zote ni za Allaah.

Kuhusiana na kuwasengenya watu ni dhambi nyingine. Wamefanya vizuri kwa njia ya kwamba wametekeleza swalah kwa mkusanyiko na wamefanya vibaya kwa njia ya kwamba wanawasengenya watu. Ni juu yao kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: uruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13398
  • Imechapishwa: 27/04/2018