Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali kwenye nguo ilio na damu na katika hali ya mtu kutokwa na damu mwilini katikati ya swalah?

Jibu: Hakuna neno mtu akiswali kwa nguo ilio na damu inayotokamana na mnyama msafi wakati akiwa hai. Ama damu ikiwa nyingi inayotoka ndani ya swalah basi swalah yake inabatilika. Kwa sababu damu ni najisi. Damu ikiwa nyingi inakuwa najisi. Hivyo itamlazimu kutoka na kuosha nguo yake na kuswali. Asipojua isipokuwa baada ya swalah basi swalah yake ni sahihi.

Swali: Je, swalah yake ni sahihi sawa ikiwa inatoka mwilini mwake au kutoka kwa mnyama?

Jibu: Ikiwa damu inatoka kwa mnyama mwenye kuliwa au kwa msemo mwingine damu inayobaki kwenye nyama inayoliwa, hiyo ni safi. Ama ikiwa ni damu yenye kuchuruzika, inatoka kwa mtu mwenyewe au kutoka kwa mnyama asiyeliwa basi hiyo ni najisi ikiwa nyingi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/287)
  • Imechapishwa: 09/01/2020