Swalah kwa aliyelala koma/ICU miezi mitatu


Swali: Niliingizwa hospitali na nikakaa huko kwa takriban muda wa miezi mitatu na sikuswali swalah za faradhi kwa sababu nilikuwa nimepoteza fahamu kabisa kwenye koma/ICU. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Mtu mfano wako amenyanyuliwa kalamu. Kulazimikiwa kwa ´ibaadah kumefungamana na kuwa na akili. Mtu anapolazwa koma/ICU fahamu zake zinamwondoka. Hivyo si swalah wala funga ya Ramadhaan haimlazimu na wewe uko katika hali kama hii. Ni mwenye kupewa udhuru. Mfano wako ni kama wa mtumzima aliyetokwa na akili au mwendawazimu. Hakuna kinachowalazimu.

Unapoamka na kupata fahamu ndio unaanza tena kutenda. Wewe punde tu pale unapoamka ndio unaanza tena kufanya matendo. Kuhusu ule muda wote ambao ulikuwa umelazwa koma/ICU hakuna kinachokulazimu. Kwa sababu kipindi hicho huna akili za kupambanua kati ya amri na makatazo ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4267/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D9%84%D9%85%D9%86-%D9%85%D9%83%D8%AB-%D9%81%D9%8A-%D8%BA%D9%8A%D8%A8%D9%88%D8%A8%D8%A9-%D8%B7%D9%88%D9%8A%D9%84%D8%A9
  • Imechapishwa: 28/05/2020