Swali: Kuna kidhibiti kipi kwa kukaa juu ya kiti na kuswali? Lililo bora zaidi ni kukaa katika ardhi na kuswali?

Jibu: Haifai kwake kuswali hali ya kuwa amekaa juu ya kiti ikiwa anaweza kuswali kwa kukaa katika ardhi. Asikae na kuswali juu ya kiti isipokuwa tu pale ambapo atashindwa kukaa katika ardhi. Katika hali hii ni sawa akakaa juu ya kiti na kuswali hali ya kuegama wakati wa Rukuu´ na Sujuud na afanye Sujuud kushuka zaidi kuliko Rukuu´.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-qrran-19-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020