Swalah inayomzuia mtu machafu na maovu

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ

“Ambao wanaamini ghaibu na husimamisha swalah na hutoa sehemu ya vile tulivyowaruzuku.”[1]

Hakusema:

“Wanaswali.”

kwa sababu haitoshi peke yake kule kuleta sura yake ya nje. Kusimamisha swalah ni kule kuisimamisha kiunje kwa kukamilisha nguzo zake, mambo yake ya wajibu na sharti zake. Kuisimamisha kuindani ni kule kusimamisha roho yake ambako ni kuuhudhurisha moyo juu yake na kuzingatia yale anayoyasema. Hii ndio swalah ambayo Allaah amesema juu yake:

إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنْكَرِ

“Hakika si vyenginevyo swalah inazuia machafu na maovu.”

Swalah kama hii ndio inayopelekea kupata thawabu. Mtu hapati thawabu kutoka katika swalah yake isipokuwa kwa kiasi cha yale atayoyaelewa. Neno swalah hapa limekusanya zile za faradhi na zile za sunnah.

[1] 02:03

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, sid. 30
  • Imechapishwa: 05/05/2020