Swalah iliyompita mtu inailipa wakati wowote

Swali: Je, inafaa kulipa swalah katika wakati wowote kwa yule aliyepitwa na swalah ndani ya wakati wake?

Jibu: Aliyepitwa na swalah ndani ya wakati wake basi itafaa kwake kuilipa wakati wowote ataweza. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayesahau kuswali au akapitikiwa na usingizi basi aiswali atapokumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]

Swalah iliyompita mtu inalipwa wakati wowote. Swalah kama hiyo haina wakati uliokatazwa. Matamko la muulizaji kuna ujumla ndani yake. Kwa sababu amesema “kulipa swalah”. Kilichotakikana ni yeye kusema “kulipa swalah iliyompita”.

[1] Muslim (684) na al-Bukhaariy (597).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/304)
  • Imechapishwa: 08/01/2020