Swali: Niko katika Rak´ah ya kwanza ya Sunnah halafu kukakimiwa swalah. Je, niikate?

Jibu: Ikiwa unaweza kuikhafifisha na ukatoa Tasliym kabla imamu hajarukuu, fanya hivo. Lakini ikiwa imamu atarukuu kabla ya wewe kukamilisha swalah yako, ikate.

Swali: Nitole Tasliym upande wa kulia na wa kushoto endapo nitaikata?

Jibu: Hukuikamilisha. Tasliym inatolewa wakati wa kukamilisha:

“Ufunguzi wa swalah ni twahara. Uharamu wake ni Takbiyr na uhalali wake ni Tasliym.”[1]

[1] Abu Daawuud (618), at-Tirmidhiy (3), Ibn Maajah (275), ash-Shaafi´iy (1/34), Ibn Abiy Shaybah (1/208) na Ahmad (1006). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (55).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (6) http://alfawzan.af.org.sa/node/14379
  • Imechapishwa: 26/11/2016